Kanisa hai ni mkusanyiko wa wacha Mungu, waliokubali kuongozwa na Mungu pamoja na Roho Mtakatifu
Kanisa la jinsi hiyo linao MSINGI ambao kwa huo linaishi na kutegemezwa
Mathayo 16:18 “Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya MWAMBA huu nitalijenga Kanisa langu; Wala milango ya kuzimu haitalishinda”
Neno la msingi hapo ni JUU YA MWAMBA HUU. tunaona hapo YESU Kristo anazungumzia habari ya kulijenga Kanisa juu ya mwamba,; mwamba ule unasimama Kama MSINGI wa Kanisa
Katika mazungumzo hayo MWAMBA unaotajwa pale pamapotarajiwa kujengwa kanisa ni YESU KRISTO kwani yeye ndiye jiwe juu la pembeni. Lakini pia tukumbuke kuwa YESU KRISTO ni Neno
Yohana 1:1,14 “Hapo mwanzo kulikua na Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno alikuwa alifanyika mwili, akakaa kwetu ; nasi tukauona utukufu wake, utukufu Kama wa mwana pekee atokaye kwa Baba;. Amejaa neema na Kweli”
YESU KRISTO mwenyewe anatutaka tujengwe katika MWAMBA kwakuwa sisi ndio Kanisa halisi(1Korintho 6:19; 2Korintho6:16) hivyo Basi alisema “Basi Kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye ajili, aliyejenga nyumba yake juu ya MWAMBA; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya MWAMBA” ( Mathayo 7:24-25)
Kumekuwepo na fundisho potofu linalofanywa na mitume na manabii wa siku za leo, wakitumia vibaya andiko hili “Mmejengwa juu ya MSINGI wa mitume na manabii, naye KRISTO YESU mwenyewe ni jiwe juu la pembeni” hilo ndiyo andiko ambalo wanalitafsiri kimakosa wakidhani ya kwamba linazungumzia kuwa mitume ndiyo MSINGI wa kanisa. Andiko hili linazungumzia Kanisa kujengwa juu ya fundisho na Imani ya mitume na manabii
Jambo mhimu kujiuliza hapo ni “Je imani na fundisho lao NI lipi?
Fundisho na Imani ya mitume na manabii ni KRISTO” ndiyo maana hata katika mstari huo unamaliza kwa kusema na KRISTO YESU mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni
Pia Paulo annaelezea kuwepo kwa msingi mmoja pekee na watumishi wengine wote wanajenga juu ya msingi huo anaposema “Maana MSINGI mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, YESU KRISTO”. (1Kor 3:11). Hivyo tunapaswa kujengwa katika KRISTO YESU na hiyo ndiyo Imani na fundisho la mitume
Kuhubiri vitu vingine ni kukengeuka na kutafuta laana bure zaidi Sana kukosa mbingu angalia haya maandiko mwana wa Mungu
Pia kiini Cha Fundisho la mitume na kiini Cha INJILI ni KRISTO YESU mwenyewe na mitume walifundisha juu ya hiyo na watu wanapaswa kufundishwa huyo na kumtegemea huyo “Basi ndugu zangu nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, na kwa hiyo mnaololewa; ikiwa mnayashika Sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure. Kwa maana niliwatolea ninyi hapo mwanzo yake noliyoyapokea Mimi mwenyewe, ya kuwa KRISTO alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, Kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, Kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wake thenashara;” (1Kor15:1-5) hivyo basi inatupasa kumhubiri Kristo so vinginevyo
“Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi Yeye(KRISTO) aliyewaita katika neema ya KRISTO, na kugeukia INJILI ya nanna nyingine. Wala so nyingine; Lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeunza injili ya KRISTO. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na Sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe” (Wagalatia 1:6-9)
Leo Kuna INJILI za nanna nyingine nyingi yaani injili za vitu wahubiri wakidai mafunuo mapya huu no uongo na ni kufanya biashara kwa jina la YESU KRISTO. Kwako wewe mtu wa Mungu mshirika unayetafuta Mungu usidanganywe na hekima na Elimu na ujanja wa hawa watu bali elewa kuwa Mungu awezaye kukufanyia yote kinachotakiwa no kumwamini YESU KRISTO pekee yake
“Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa Elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, Wala so kwa jinsi ya KRISTO” (Wakolosai 2:8) epuka kupigwa pesa unapotezwa mwana wa Mungu
Jiepushe na ujinasue na mtego wa shetani kwa kutumia waalimu, manabii, na wachungaji wa uongo; Bali mtunainie Mungu kupitia YESU KRISTO pekee Wala so mafuta Wala vitambaa Wala maji Wala chumvi na chochote Bali KRISTO; kwani YESU KRISTO ndiye aliyekufa kwa ajili yako na ndiye aliyelango la mbinguni
Yohana 10:1-2,7-10[1]Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi. [2]Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.[7]Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.[8]Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia.[9]Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.[10]Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
Rafiki yangu mpe YESU KRISTO Maisha yako afanyike kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako mkaribishe yeye ni Rafiki mwaminifu ni mwenye huruma, upendo na ukarimu. Ni mponyaji na mfariji wakati wa mateso haijalishi shida na taabu unayoipitia mgeukie Kristo atakuinua tena nimemwona akitenda katika maisha yangu na kwa wengine pia
Maombi
Fuatisha MANENO haya Kwa kumaanisha KRISTO atatenda jambo
Baba katika jina la YESU KRISTO nakuja mbele zako Mimi ni mwenye dhambi nahitaji kutakaswa na kusafishwa nawe ingiza ndani yangu Leo ufanyike BWANA na MWOKOZI wa maisha yangu
Nakaataa matendo ya shetani na kazi zake zote, navunja maagano na Giza Kwa damu Yako YESU KRISTO safisha ndani yangu na unipe Roho wako aniongoze daima katika jina la YESU KRISTO Amen
Mungu akubariki rafiki tafuta kanisa lilaokiri wokovu na linalofuata maadili ya Kristo
By mwalimu Anselemi Mashimba Alloyce 0747-251 929
Good lesson