MAISHA YA MITUME 12 WA YESU KRISTO

MAISHA YA MITUME 12 WA AGANO JIPYA

Katika somo hili tutajifunza kwa kufuata vipengele vifuatavyo:-

  1. Asilia na maana ya neno Mtume
  2. Fundisho na imani ya mitume
  3. Maisha na kifo cha kila mtume
  4. Mitume katika kanisa la sasa

A:- ASILIA NA MAANA YA NENO MTUME
MTUME ni neno lililotokana na neno la kigiriki Apostolos lenye maana ya “ALIYETUMWA”. Hivyo mtume ni mtu ALIYETUMWA kupeleka ujumbe wa injili ya Yesu Kristo.
Mitume walihubiri/kueneza mafundisho ya kibiblia kuhusu imani ya dini ya kikristo na nguvu ya upendo wa Mungu kwa mwanadamu. Dhamira ya mtume ni kumhubiri Yesu Kristo, kazi yake ya ukombozi wa mwanadamu, maisha yake, kifo chake na kufufuka kwake (1 Wakorintho 15:1- 8
Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure. Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;
na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.)

NANI ALIANZISHA KIKUNDI HIKI?
Kikundi hiki cha mitume kilianzishwa na Yesu Kristo mwenyewe. Mitume hawa walikuwa 12 na walikuwa watu wa karibu sana na YESU KRISTO na walikuwa wanamsaidia sana katika kueneza injili
Mitume hao ni wafuatao:-
1: Simon Petro. 2: Simon Mkananayo(Zelothe
3: Yakobo mwana wa Zebedayo
4: Bartholomayo 5: Yohana mwana wa Zebedayo
6: Tomaso 7: Filipo
8: Mathayo (Lawi)
9: Yakobo mwana wa Alfayo
10: Thadayo/Yuda wa Zelote
11: Andrea 12: Yuda Iskariote
Mathayo 10:2-4, Mathayo 4:18-22, Marko 1: 16-20, 3:13-19

Mitume walikuwa na kazi ya
A.Kuhubiri ufalme wa Mungu ( Mathayo 10: 7)
B. Kuponya wagonjwa na walioonewa na shetani (Mathayo 10: 8)

Katika nyaraka zake Paulo anajitambulisha Kuwa pia MTUME wa mataifa aliyeitwa na YESU KRISTO aliyefufuka
(Matendo ya Mitume 9:15 – 16
Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu)
Paulo aliingia kwenye orodha ya mitume kutokana na kuitwa na Yesu Kristo akiwa anakwenda Dameski na kuagizwa kupeleka injili kwa mataifa kwani sifa ya Kuwa mtume ni Kuwa umewahi kumwona YESU KRISTO Paulo alimwona YESU KRISTO (1 Wakorintho 9:1- 2
Je! Mimi si huru? Mimi si mtume? Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Ninyi si kazi yangu katika Bwana?
Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, lakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana ninyi ndinyi muhuri ya utume wangu katika Bwana.)

Itaendelea tena siku nyingine

MSHUKURU MUNGU KWA HURUMA ZAKE

Maombolezo 3:22-23
22 Ni huruma za Bwana kwamba hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi. 23 Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu
MAELEZO

Ni nini kilikutegemeza usiku? Je! Utapata nini leo? Ni nini kitakachokuwezesha kufikia, hata kufanikiwa, katika siku zijazo? Huruma za BWANA. Rasilimali hizi nzuri hazijaisha kabisa! Kila siku mpya huleta ugavi mpya wao. Mungu ni mwaminifu kuhakikisha tunazo kila siku. Mungu asifiwe kwa kuifanya dunia yetu iwe mpya na iwe safi kila siku mpya
OMBI

Asante, Mungu mtakatifu na Baba mwenye upendo, kwa kunitegemeza usiku kucha na kuniahidi siku isiyo na mwisho mwishoni mwa safari yangu ya maisha. Naomba wewe, Baba yangu wa mbinguni, upate upendo na sifa kwenye midomo yangu na moyoni mwangu wakati wote. Kwa jina la Yesu. Amina.

NI WAKATI WA ZAMU YAKO

Mara nyingi tunaishi kwa vipindi na ZAMU katika dunia tuliyopo na wakati was ZAMU unapowaidia tunakuwa na majukumu ya kufanya katika kipindi hicho pasipo kujali idadi na Hali tuliyonayo

Maandiko yanasema “msiogope enyi kundi dogo kwa kuwa Baba yenu ameona vyema kuwapa ule ufalme” (Luka12:32). Hivyo kwa nanna yoyote na kwa idadi yoyote Mungu anakuwa ameturidhia kwa yeye huutazama moyo

Hatupaswi kunyamaza kwa sababu sisi no Chumvi na Nuru ya ulimwengu (mathayo5:13-16); Hivyo popote tulipo tunapaswa kusimama Katika ZAMU zetu vyema

Ikumbukwe kuwa Mungu anataka mtu mmoja tu atakae tenda kwa ya uaminifu (Yere 5:1; Malaki 1: 10)

Mfano: – Isaya 62:6-12

Mwana wa Mungu fanya kazi ya Bwana usiogope umeaminiwa

YESU KRISTO NI MSINGI WA KANISA HAI

Kanisa hai ni mkusanyiko wa wacha Mungu, waliokubali kuongozwa na Mungu pamoja na Roho Mtakatifu

Kanisa la jinsi hiyo linao MSINGI ambao kwa huo linaishi na kutegemezwa

Mathayo 16:18 “Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya MWAMBA huu nitalijenga Kanisa langu; Wala milango ya kuzimu haitalishinda”

Neno la msingi hapo ni JUU YA MWAMBA HUU. tunaona hapo YESU Kristo anazungumzia habari ya kulijenga Kanisa juu ya mwamba,; mwamba ule unasimama Kama MSINGI wa Kanisa

Katika mazungumzo hayo MWAMBA unaotajwa pale pamapotarajiwa kujengwa kanisa ni YESU KRISTO kwani yeye ndiye jiwe juu la pembeni. Lakini pia tukumbuke kuwa YESU KRISTO ni Neno

Yohana 1:1,14 “Hapo mwanzo kulikua na Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno alikuwa alifanyika mwili, akakaa kwetu ; nasi tukauona utukufu wake, utukufu Kama wa mwana pekee atokaye kwa Baba;. Amejaa neema na Kweli”

YESU KRISTO mwenyewe anatutaka tujengwe katika MWAMBA kwakuwa sisi ndio Kanisa halisi(1Korintho 6:19; 2Korintho6:16) hivyo Basi alisema “Basi Kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye ajili, aliyejenga nyumba yake juu ya MWAMBA; mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya MWAMBA” ( Mathayo 7:24-25)

Kumekuwepo na fundisho potofu linalofanywa na mitume na manabii wa siku za leo, wakitumia vibaya andiko hili “Mmejengwa juu ya MSINGI wa mitume na manabii, naye KRISTO YESU mwenyewe ni jiwe juu la pembeni” hilo ndiyo andiko ambalo wanalitafsiri kimakosa wakidhani ya kwamba linazungumzia kuwa mitume ndiyo MSINGI wa kanisa. Andiko hili linazungumzia Kanisa kujengwa juu ya fundisho na Imani ya mitume na manabii

Jambo mhimu kujiuliza hapo ni “Je imani na fundisho lao NI lipi?

Fundisho na Imani ya mitume na manabii ni KRISTO” ndiyo maana hata katika mstari huo unamaliza kwa kusema na KRISTO YESU mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni

Pia Paulo annaelezea kuwepo kwa msingi mmoja pekee na watumishi wengine wote wanajenga juu ya msingi huo anaposema “Maana MSINGI mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, YESU KRISTO”. (1Kor 3:11). Hivyo tunapaswa kujengwa katika KRISTO YESU na hiyo ndiyo Imani na fundisho la mitume

Kuhubiri vitu vingine ni kukengeuka na kutafuta laana bure zaidi Sana kukosa mbingu angalia haya maandiko mwana wa Mungu

Pia kiini Cha Fundisho la mitume na kiini Cha INJILI ni KRISTO YESU mwenyewe na mitume walifundisha juu ya hiyo na watu wanapaswa kufundishwa huyo na kumtegemea huyo “Basi ndugu zangu nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, na kwa hiyo mnaololewa; ikiwa mnayashika Sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure. Kwa maana niliwatolea ninyi hapo mwanzo yake noliyoyapokea Mimi mwenyewe, ya kuwa KRISTO alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, Kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, Kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wake thenashara;” (1Kor15:1-5) hivyo basi inatupasa kumhubiri Kristo so vinginevyo

“Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha upesi hivi Yeye(KRISTO) aliyewaita katika neema ya KRISTO, na kugeukia INJILI ya nanna nyingine. Wala so nyingine; Lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeunza injili ya KRISTO. Lakini ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe. Kama tulivyotangulia kusema, na Sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe” (Wagalatia 1:6-9)

Leo Kuna INJILI za nanna nyingine nyingi yaani injili za vitu wahubiri wakidai mafunuo mapya huu no uongo na ni kufanya biashara kwa jina la YESU KRISTO. Kwako wewe mtu wa Mungu mshirika unayetafuta Mungu usidanganywe na hekima na Elimu na ujanja wa hawa watu bali elewa kuwa Mungu awezaye kukufanyia yote kinachotakiwa no kumwamini YESU KRISTO pekee yake

“Angalieni mtu asiwafanye mateka kwa Elimu yake ya bure na madanganyo matupu, kwa jinsi ya mafundisho ya awali ya ulimwengu, Wala so kwa jinsi ya KRISTO” (Wakolosai 2:8) epuka kupigwa pesa unapotezwa mwana wa Mungu

Jiepushe na ujinasue na mtego wa shetani kwa kutumia waalimu, manabii, na wachungaji wa uongo; Bali mtunainie Mungu kupitia YESU KRISTO pekee Wala so mafuta Wala vitambaa Wala maji Wala chumvi na chochote Bali KRISTO; kwani YESU KRISTO ndiye aliyekufa kwa ajili yako na ndiye aliyelango la mbinguni

Yohana 10:1-2,7-10[1]Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi. [2]Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.[7]Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.[8]Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia.[9]Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.[10]Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Rafiki yangu mpe YESU KRISTO Maisha yako afanyike kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako mkaribishe yeye ni Rafiki mwaminifu ni mwenye huruma, upendo na ukarimu. Ni mponyaji na mfariji wakati wa mateso haijalishi shida na taabu unayoipitia mgeukie Kristo atakuinua tena nimemwona akitenda katika maisha yangu na kwa wengine pia

Maombi

Fuatisha MANENO haya Kwa kumaanisha KRISTO atatenda jambo

Baba katika jina la YESU KRISTO nakuja mbele zako Mimi ni mwenye dhambi nahitaji kutakaswa na kusafishwa nawe ingiza ndani yangu Leo ufanyike BWANA na MWOKOZI wa maisha yangu

Nakaataa matendo ya shetani na kazi zake zote, navunja maagano na Giza Kwa damu Yako YESU KRISTO safisha ndani yangu na unipe Roho wako aniongoze daima katika jina la YESU KRISTO Amen

Mungu akubariki rafiki tafuta kanisa lilaokiri wokovu na linalofuata maadili ya Kristo

By mwalimu Anselemi Mashimba Alloyce 0747-251 929

YESU KRISTO NI BWANA

katika dunia hii wako wengi walio maarufu na walio na nguvu lakini YESU Kristi Ana nguvu kuliko wote

Kwani Kwani jina la YESU linauweza na linaleta wokovu na ni katika jina Hilo pekee ndipo wokovu halisi unapatikana (Wafilipi 2: 9-11 “kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia jina lile lipitalo Kila jina; ili kwa jina la YESU Kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na Kila ulimi ukiri ya kwamba YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu was Mungu Baba”)

Matendo 4:12 “Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo”

Mathayo 1:21 “Naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina lake YESU, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao”