IMANI NA FUNDISHO LA MITUME

Hivyo basi kama mtu akifundishwa kimakosa atajenga imani potofu; akifundishwa kwa usahihi atajenga imani njema/sahihi
Hapa ndipo palipopelekea kuanzisha fundisho.

A: IMANI NI NINI?
IMANI ni Kuwa na uhakika wa mambo/jambo unalolitarajia hasusani jambo lisiloonekana (Waebrania 11:1
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana).
Imani mara zote huja kwa kusikia, au kufundishwa jambo fulani.
Warumi 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.

Kabla ya kujibu tuangalie kwanza maana ya FUNDISHO
Fundisho katika AGANO JIPYA linabeba maana mbili
A). Tendo la Kufundisha 1Timotheo 4:13,16,5:17; 2Timotheo 3:10,16
B). Kile kinachofundishwa
Mathayo 15:9; 2Timotheo 4:13
Hivyo basi FUNDISHO ni maagizo, taarifa au maudhui yaliyomo kwenye kile kinachofundishwa.

B: FUNDISHO LA MITUME NI NINI?

FUNDISHO LA MITUME ni maagizo ya kwanza/mapema kabisa yaliyotolewa na mitume katika kanisa la kwanza
Fundisho la mitume liligawanyika katika maeneo makuu matatu kama ifuatavyo:-
1: YESU ndiye KRISTO. Matendo ya Mitume 9:22
Sauli akazidi kuwa hodari, akawatia fadhaa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa huyu ndiye Kristo.

Matendo ya Mitume 17:2, 3
Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko sabato tatu, akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewapasha ninyi habari zake ndiye Kristo.

2: YESU amefufuka kutoka kwa wafu.
Matendo ya Mitume 1:2
hata siku ile alipochukuliwa juu, alipokuwa amekwisha kuwaagiza kwa Roho Mtakatifu wale mitume aliowachagua;

Matendo ya Mitume 1:3
wale aliowadhihirishia nafsi yake, kwa dalili nyingi, baada ya kuteswa kwake, ya kwamba yu hai, akiwatokea muda wa siku arobaini, na kuyanena mambo yaliyouhusu ufalme wa Mungu.

Matendo ya Mitume 1:22
kuanza tangu ubatizo wa Yohana, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.

Matendo ya Mitume 2:2
Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

Matendo ya Mitume 2:3
Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

Matendo ya Mitume 2:23
mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;

Matendo ya Mitume 2:24
ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.

Matendo ya Mitume 2:2
Kukaja ghafula toka mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi.

Matendo ya Mitume 2:3
Kukawatokea ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao.

Matendo ya Mitume 2:23
mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;

Matendo ya Mitume 2:24
ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.

Matendo ya Mitume 2:32
Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.

3: WOKOVU inapatikana kupitia jina la Yesu kristo pekee. Matendo ya Mitume 4:12
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.

Matendo ya Mitume 3:16
Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.

Wakati wa kuhubiri fundisho hilo na kweli hizo tatu waliambatanisha na fundisho la IMANI KIYAHUDI ambayo msingi wake ni AGANO la Kale kuonyesha uvuvio na kutimizwa kwa agano la Kale. Soma mahubiri ya Petro, Stephano na Paulo ili uone namna ambavyo mtiririko ulikuwa na namna ambavyo agano la Kale limeungana na AGANO JIPYA
Matendo ya Mitume 2:14
Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti yake, akawaambia, Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu, lijueni jambo hili, mkasikilize maneno yangu.

Matendo ya Mitume 2:15
Sivyo mnavyodhani; watu hawa hawakulewa, kwa maana ni saa tatu ya mchana;

Matendo ya Mitume 2:16
lakini jambo hili ni lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yoeli,

Matendo ya Mitume 2:17
Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto.

Matendo ya Mitume 2:18
Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.

Matendo ya Mitume 2:19
Nami nitatoa ajabu katika mbingu juu, na ishara katika nchi chini, damu na moto, na mvuke wa moshi.

Matendo ya Mitume 2:20
Jua litageuka kuwa giza, na mwezi kuwa damu, kabla ya kuja ile siku ya Bwana iliyo kuu na iliyo dhahiri.

Matendo ya Mitume 2:21
Na itakuwa kila atakayeliitia jina la Bwana ataokolewa.

Matendo ya Mitume 2:22
Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;

Matendo ya Mitume 2:23
mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;

Matendo ya Mitume 2:24
ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.

Matendo ya Mitume 2:25
Maana Daudi ataja habari zake,
Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote,
Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike.

Matendo ya Mitume 2:26
Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa,
ulimi wangu ukafurahi;
Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini.

Matendo ya Mitume 2:27
Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu;
Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.

Matendo ya Mitume 2:28
Umenijuvisha njia za uzima;
Utanijaza furaha kwa uso wako.

Matendo ya Mitume 2:29
Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.

Matendo ya Mitume 2:30
Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi;

Matendo ya Mitume 2:31
yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu.

Matendo ya Mitume 2:32
Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.

Matendo ya Mitume 2:33
Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.

Matendo ya Mitume 2:34
Maana Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye mwenyewe anasema,
Bwana alimwambia Bwana wangu,
Keti upande wa mkono wangu wa kuume.

Matendo ya Mitume 2:35
Hata nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.

Matendo ya Mitume 2:36
Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa Bwana na Kristo.

(Soma pia Matendo ya mitume 5:29-32; 7:2-52)

Ndani ya fundisho la mitume kulikuwa na kweli kadha ambazo zilikuwa zikitiliwa mkazo; baadhi yake ni
1: Kristo alijitoa kufa msalabani ili kutimiza kusudi la Mungu la ukombozi.
Matendo ya Mitume 2:22
Enyi waume wa Israeli, sikilizeni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mtu aliyedhihirishwa kwenu na Mungu kwa miujiza na ajabu na ishara, ambazo Mungu alizifanya kwa mkono wake kati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua;

Matendo ya Mitume 2:23
mtu huyu alipotolewa kwa shauri la Mungu lililokusudiwa, na kwa kujua kwake tangu zamani, ninyi mkamsulibisha kwa mikono ya watu wabaya, mkamwua;

(Soma pia Matendo ya mitume 3:18-21)

2: YESU KRISTO yu hai alifufuka kutoka kwa wafu.
Matendo ya Mitume 2:24
ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.

Matendo ya Mitume 2:25
Maana Daudi ataja habari zake,
Nalimwona Bwana mbele yangu siku zote,
Kwa kuwa yuko upande wa mkono wangu wa kuume, nisitikisike.

Matendo ya Mitume 2:26
Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa,
ulimi wangu ukafurahi;
Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini.

Matendo ya Mitume 2:27
Kwa maana hutaiacha roho yangu katika kuzimu;
Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.

Matendo ya Mitume 2:28
Umenijuvisha njia za uzima;
Utanijaza furaha kwa uso wako.

Matendo ya Mitume 2:29
Waume, ndugu zangu, mniwie radhi, niseme kwa ujasiri mbele yenu habari za baba yetu mkuu, Daudi, ya kuwa alifariki akazikwa, na kaburi lake liko kwetu hata leo.

Matendo ya Mitume 2:30
Basi kwa kuwa ni nabii, akijua ya kuwa Mungu amemwapia kwa kiapo, ya kwamba katika uzao wa viuno vyake atamketisha mmoja katika kiti chake cha enzi;

Matendo ya Mitume 2:31
yeye mwenyewe akitangulia kuyaona haya, alitaja habari za kufufuka kwake Kristo, ya kwamba roho yake haikuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuona uharibifu.

Matendo ya Mitume 2:32
Yesu huyo Mungu alimfufua, na sisi sote tu mashahidi wake.

3: Yesu Kristo yuko mkono wa kuume wa Mungu, mbinguni

Matendo ya Mitume 1:9
Akiisha kusema hayo, walipokuwa wakitazama, akainuliwa, wingu likampokea kutoka machoni pao.
Matendo ya Mitume 2:33
Basi yeye, akiisha kupandishwa hata mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu, amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.

Matendo ya Mitume 2:34
Maana Daudi hakupanda mbinguni; bali yeye mwenyewe anasema, Bwana alimwambia Bwana wangu, Keti upande wa mkono wangu wa kuume.

Matendo ya Mitume 2:35
Hata nitakapowaweka adui zako chini ya miguu yako.

4: YESU ni BWANA na ndiye KRISTO
Matendo ya Mitume 2:36
Basi nyumba yote ya Israeli na wajue yakini ya kwamba Mungu amemfanya Yesu huyo mliyemsulibisha kuwa BWANA na KRISTO.

5: Imani katika jina la Yesu Kristo, ina nguvu na huleta uponyaji, wa kimwili na kiroho
Matendo ya Mitume 3:16
Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote.

Matendo ya Mitume 3:17
Basi sasa, ndugu, najua ya kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda.

Matendo ya Mitume 3:18
Lakini mambo yale aliyohubiri Mungu tangu zamani kwa kinywa cha manabii wake wote, ya kwamba Kristo wake atateswa, ameyatimiza hivyo.

Matendo ya Mitume 3:19
Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;

Matendo ya Mitume 3:20
apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani;
Matendo ya Mitume 9:34
Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka.

Matendo ya Mitume 10:43
Huyo manabii wote humshuhudia, ya kwamba kwa jina lake kila amwaminiye atapata ondoleo la dhambi.

Tangu kipindi cha MITUME kulikuwa na upotoshaji na kupigwa vita sana dhidi ya imani na matumizi ya jina la Yesu kristo
(Soma, Matendo ya mitume 4:13-22; 5:27-29,40)

Hata sasa katika zama zetu wako wahubiri, manabii, mitume, waalimu na wachungaji ambao kwa namna moja ama nyingine wanajaribu kuonyesha kwamba jina la Yesu kristo halitoshi ndiyo maana wanaweka viambata ambavyo wanaweka kama vile chumvi, mafuta, vitambaa, picha zao, n.k, mambo hayo ni kuturudisha agano la Kale yaani torati ambapo AGANO LA KALE ni kivuli. Kwa nini kujitia kwenye kongwa tena na kutumia kitu mbadala wakati kitu halisi kipo?
Wakolosai 2:13
Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote;

Wakolosai 2:14
akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;

Wakolosai 2:15
akiisha kuzivua enzi na mamlaka, na kuzifanya kuwa mkogo kwa ujasiri, akizishangilia katika msalaba huo.

Wakolosai 2:16
Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

Wakolosai 2:17
mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.

6: Mamlaka ya Yesu Kristo kusamehe dhambi
Matendo ya Mitume 5:31
Mtu huyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toba na msamaha wa dhambi.

7: Ujazo na utendaji wa Roho Mtakatifu
Matendo ya Mitume 8:14
Na mitume waliokuwako Yerusalemu, waliposikia ya kwamba Samaria imelikubali neno la Mungu, wakawapelekea Petro na Yohana;

Matendo ya Mitume 8:15
ambao waliposhuka, wakawaombea wampokee Roho Mtakatifu;

Matendo ya Mitume 8:16
kwa maana bado hajawashukia hata mmoja wao, ila wamebatizwa tu kwa jina lake Bwana Yesu.

Matendo ya Mitume 8:17
Ndipo wakaweka mikono yao juu yao, nao wakampokea Roho Mtakatifu.

(Soma, Matendo ya mitume 8:29; 10:44-47)
8: Ubatizo wa maji mengi
Matendo ya Mitume 8:35
Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.

Matendo ya Mitume 8:36
Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? [

Matendo ya Mitume 8:37
Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, inawezekana. Akajibu, akanena, Naamini ya kwamba Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu.]

Matendo ya Mitume 8:38
Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza.

Matendo ya Mitume 8:39
Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.

Matendo ya Mitume 10:47
Ni nani awezaye kuzuia maji, hawa wasibatizwe, watu waliopokea Roho Mtakatifu vile vile kama sisi?

Matendo ya Mitume 10:48
Akaamuru wabatizwe kwa Jina lake Yesu Kristo. Ndipo wakamsihi azidi kukaa siku kadha wa kadha.

9: Tumaini la mbingu mpya na nchi mpya
2 Petro 3:13
Lakini, kama ilivyo ahadi yake, mnatazamia mbingu mpya na nchi mpya, ambayo haki yakaa ndani yake.

Hilo ndilo fundisho la mitume ambalo kanisa la leo limejengwa juu yake
Mathayo 16:16
Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.

Mathayo 16:17
Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

Mathayo 16:18
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.

Mathayo 16:19
Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
1 Petro 2:4
Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.

1 Petro 2:5
Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.

1 Petro 2:6
Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko
Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima,
Na kila amwaminiye hatatahayarika.

1 Petro 2:7
Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,
Jiwe walilolikataa waashi,
Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

1 Petro 2:8
Tena,
Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha.
Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.

1 Petro 2:9
Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

1 Petro 2:10
ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.

Mwamba ni YESU KRISTO hivyo kanisa limejengwa juu ya Kristo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *