MAISHA YA MITUME 12 WA AGANO JIPYA
Katika somo hili tutajifunza kwa kufuata vipengele vifuatavyo:-
- Asilia na maana ya neno Mtume
- Fundisho na imani ya mitume
- Maisha na kifo cha kila mtume
- Mitume katika kanisa la sasa
A:- ASILIA NA MAANA YA NENO MTUME
MTUME ni neno lililotokana na neno la kigiriki Apostolos lenye maana ya “ALIYETUMWA”. Hivyo mtume ni mtu ALIYETUMWA kupeleka ujumbe wa injili ya Yesu Kristo.
Mitume walihubiri/kueneza mafundisho ya kibiblia kuhusu imani ya dini ya kikristo na nguvu ya upendo wa Mungu kwa mwanadamu. Dhamira ya mtume ni kumhubiri Yesu Kristo, kazi yake ya ukombozi wa mwanadamu, maisha yake, kifo chake na kufufuka kwake (1 Wakorintho 15:1- 8
Basi, ndugu zangu, nawaarifu ile injili niliyowahubiri; ambayo ndiyo mliyoipokea, na katika hiyo mnasimama, na kwa hiyo mnaokolewa; ikiwa mnayashika sana maneno niliyowahubiri isipokuwa mliamini bure. Kwa maana naliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko; na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko;
na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Thenashara; baadaye aliwatokea ndugu zaidi ya mia tano pamoja; katika hao wengi wanaishi hata sasa, ila baadhi yao wamelala; baadaye akamtokea Yakobo; tena na mitume wote; na mwisho wa watu wote, alinitokea mimi, kama ni mtu aliyezaliwa si kwa wakati wake.)
NANI ALIANZISHA KIKUNDI HIKI?
Kikundi hiki cha mitume kilianzishwa na Yesu Kristo mwenyewe. Mitume hawa walikuwa 12 na walikuwa watu wa karibu sana na YESU KRISTO na walikuwa wanamsaidia sana katika kueneza injili
Mitume hao ni wafuatao:-
1: Simon Petro. 2: Simon Mkananayo(Zelothe
3: Yakobo mwana wa Zebedayo
4: Bartholomayo 5: Yohana mwana wa Zebedayo
6: Tomaso 7: Filipo
8: Mathayo (Lawi)
9: Yakobo mwana wa Alfayo
10: Thadayo/Yuda wa Zelote
11: Andrea 12: Yuda Iskariote
Mathayo 10:2-4, Mathayo 4:18-22, Marko 1: 16-20, 3:13-19
Mitume walikuwa na kazi ya
A.Kuhubiri ufalme wa Mungu ( Mathayo 10: 7)
B. Kuponya wagonjwa na walioonewa na shetani (Mathayo 10: 8)
Katika nyaraka zake Paulo anajitambulisha Kuwa pia MTUME wa mataifa aliyeitwa na YESU KRISTO aliyefufuka
(Matendo ya Mitume 9:15 – 16
Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu)
Paulo aliingia kwenye orodha ya mitume kutokana na kuitwa na Yesu Kristo akiwa anakwenda Dameski na kuagizwa kupeleka injili kwa mataifa kwani sifa ya Kuwa mtume ni Kuwa umewahi kumwona YESU KRISTO Paulo alimwona YESU KRISTO (1 Wakorintho 9:1- 2
Je! Mimi si huru? Mimi si mtume? Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Ninyi si kazi yangu katika Bwana?
Kwa maana ikiwa mimi si mtume kwa wengine, lakini ni mtume kwenu ninyi; kwa maana ninyi ndinyi muhuri ya utume wangu katika Bwana.)
Itaendelea tena siku nyingine